Mapacha Na maamuzi ya kuja na njia za panya.

13256517_1056176057763010_7362945716759446169_n

Mapacha Na maamuzi ya kuja na njia za panya.

PKP ikiwa na maana ya Pasu Kwa Pasu waite Mapacha Maujanja Saplaya ambao ni moja kati ya wakali wa muziki wa hiphop, pia ni wanaharakati ambao kupitia project yao ya Ant Virus waliweza kubaadilisha mengi mabaya katika muziki wa kizazi kipya.

Mapema wakiongea na Team Tizneez hawakusita kusema “Tumeamua kuja na na njia za panya unaweza ukastuka kidogo ila ni album yetu ambayo tutauza wenyewe tu. Tumeipa jina la njia za panya maana ni jinsi ambavyo tumepanga vile ambavyo tutauza.

Kutakuwa na nyimbo nyingi na nzuri maana tumefanya na watarishaji bora wote, pia ni nyimbo ambazo hazijawahi kutoka katika album hii wimbo ulitoka ni Kipande flani feat becka Title na Linex tu.

Hivyo mashabiki wetu wajue tunakuja na mengi mazuri ila album ya njia za panya itakufikia popote pale ulipo.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez