Mafanikio ya wasanii wa kizazi kipya mbona yanatia shaka?

Mafanikio ya wasanii wa kizazi kipya mbona yanatia shaka?

Ni kawaida sasa kuona wasanii wa muziki wa kizazi kipya hasa wa Bongo fleva wakionyesha vitu vingi vya thamani ambavyo wanamiliki.

Lakini katika upande wa pili malalamiko juu ya kuibiwa kazi zao, kupewa pesa ndogo kwenye matumbuizo mengi, na hata kuimbishwa bure ni jambo la kawaida kwao.

Licha ya changamoto hizo lakini kupitia mitandao ya kijamii wameendelea kuonekana ni wenye mafanikio ya kiwango cha juu. Pia ni jambo la kawaida kusema amefanya video ya pesa nyingi mno tena Afrika ya Kusini.

Katika vijiwe vya wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kumekuwepo na hisia mbalimbali juu yao. Wapo ambao husema wanafanya biashara ambazo ni haramu, wapo ambao husema wengine hujiusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Ila sisi ni mwiko kuandika vitu kwa hisia isipokuwa uhalisia wa kweli. Duniani kote katika biashara ya muziki hutegemea zaidi mauzo ya album, lakini kwetu hakuna kabisa biashara hiyo. Lakini pia swala la matumbizo licha ya hapa kwetu wasanii wengi hufanya matumbuizo ya bure maana wengi wao hawana uwezo wa kuandaa maonyesho yao wenyewe, na kama akiandaa mdau basi mdau hupanga pesa ya kumlipa msanii sio msanii kupanga pesa anayotaka kulipwa.

Je mafanikio yao ambayo wanasema wanayo na hata kutuonyesha katika mitandao ya kijamii wanatoa wapi?

Unaweza kuta msanii ametoa nyimbo tatu lakini baada ya hapa huanza kuishi kifalme, ni kweli muziki wetu umefikia katika mafanikio makubwa hata ukitoa nyimbo tatu?

Ukweli uko wapi kwenye jambo hili?

Tupe maoni yako hapa chini

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez