MAEMBE VITALI SIJATEKWA ILA SIPO HURU,NAISHI KARIBU NA KIFO

vitali_maembe
Sumu ya teja ni moja kati ya nyimbo zake zilizompatia umaarufu mkubwa Vitali Maembe hapa inchini na nje ya nchi.
Rushwa,na vuma ni muendelezo wa nyimbo zake ambazo zimekuwa zikibeba mafunzo na ujumbe mzito,Vitali amekuwa kinara wa kutunga tungo zenye kueleimisha jamii licha ya kuburudisha pia.
Baada ya kuwa kimya kwa siku kadhaa Vital Maembe ameamua kuweka wazi baada ya kimya cha muda mfupi.Vitali alisema “Sijatekwa ila sipo Huru, Nipo mbali na ni naelekea mbali zaidi.
Ndugu zangu! Watu wote hatuishi mbali na Mauti, lakini Mimi Vitali Maembe leo naishi karibu kabisa na kifo, natembea kwenye ukingo wa Uhai wangu lakini bado sijashindwa kuyabeba matumaini ya wengi wanaonitegemea, sijilegezi na wala sitajilegeza nikatizwe uhai wangu kirahisi kwa uzembe wangu.

Poleni Sana Rafiki zangu, wanangu na wanafunzi wangu, nilipenda nisiwasiliane nanyi ili nisiwape nafasi watu kwenye nia mbaya, lakini nalazimika kufanya hivyo ili niwaondoe mashaka kwa kutoweka kwangu kwa siku kadhaa.

Naomba mfahamu kuwa sijatekwa na sijaumizwa sehemu yoyote zaidi ya kusononeshwa moyo wangu kwa kuona kuwa kuna watu wanaonivizia wanidhuru kutokana kazi yangu ya Muziki.

Naomba niwatakie Uchaguzi mwema na wa Amani, nendeni kwenye kampeni za vyama vyote kwa kadri mnavyoweza, wasikilizeni wagombea wa vyama vyote na muamue vema kwa hatma njema ya Taifa lenu, mkumbuke kuwa kura yako Moja Inakuamulia wewe na yule aliyeshindwa kupiga kwakuwa hajatimiza Umri, wenye matatizo ya Akili, wagonjwa mahututi na wenye Dharula nzito.

Leo nimepata msaada wa mawasiliano lakini sitadumu hewani, kila nitakapopata fursa ntakuwa nawasiliana nanyi, tuombeane usalama na uhai. Sikimbii wala siogopi vita hii, nikisema kuwa sikujua kuwa Muziki wangu utachukiwa na kuhatarisha Maisha yangu ntakuwa muongo, nilijua na nipo tayari kwa vita baada ya Uchaguzi. Mungu alinipa kazi na nimeikubali, Nitapigana kwa jina la Mungu wa waafrika na Mungu atashinda.

Unaweza kuwa rafiki yetu facebook.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez