MAEMBE VITALI AWATAKA CHANNEL TEN KUACHA KUPIGA NYIMBO ZAKE

10983419_1599366313608284_3004310748487957575_n

Maembe Vitali ni moja kati ya wasanii wachache wanaofanya vyema katika muziki wa asili, ambapo pia imekuwa kawaida kuonekana zaidi katika matumbuizo ya bongo fleva. Sumu ya teja ni miongoni mwa nyimbo zake zilizompa umaarufu ndani na nje ya nchi pia.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook msanii Vitali Maembe hakusita kuweka hisia zake juu ya ituo cha runinga Channel Ten ambapo ameandika “Channel ten tz na Utalii wa ndani, sitaki ugomvi na mtu!
‘Tuheshimiane’
Ni Mwaka mwaka wa tatu sasa kituo cha Television cha Channel Ten mmekuwa mkirusha kipindi cha utalii wa ndani kikisindikizwa Nyimbo zangu mbali mbali.
Mwanzoni mlianza kuandika kaimba nani, baadaye mkaanza kutaja majina ya watu wengine, nasasa mmeuchuna mnaona kuwa ni Nyimbo zenu au zimejitunga zikajirekodi zenyewe?
Hamnilipi hamuwasiliani nami.
Niliwatumia ujumbe mkajifanya hamna milango ya fahamu. Hamna heshima na kazi za watu wala hamna maadili ya kazi yenu.
Au ndiyo ‘baniani mbaya lakini Kiatu chake dawa’?
Kuanzia sasa sitaki kusikia tena Nyimbo zangu kwenye kipindi chenu.
Sio ombi.