MADEE ATOLEA MAELEZO AHADI YAKE YA KUCHOMA GARI

Mdeeee-2222

Mkali tokea pande za Manzese Madee ambaye ni kinara katika muziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri tangu alipoingia katika ramani ya muziki miaka ya 2000.

Katika haki isiyo ya kawaida jana msanii huyu Madee aliweka ahadi kuptia mtandao wa picha Instagram ambapo aliandika “Kama chelsea ikimfunga Arsenal basi nitachoma gari langu moja moto”

Mpaka mpira unaisha katika mechi hiyo iliyowakutanisha Chelsea na Arsenal,Cheslsea ilitoka kifua mbele kwa kumfunga Arsenal bao 1 kwa 0.

Madee leo hii ameamua kutoa ufafanuzi kupitia mtandao wa twitter ambapo alisema “Sina utajiri huo mpaka kufikia hatua ya kuchoma gari, na hata kama ningekuwa tajiri vipi nisingewesa kufanya upumbavu huo.”

Tweet yake chini hapa

Capture

www.tizneez.com

Twitter tizneez

facebook tizneez

Instagram tizneez