MAALUM KWA WASANII WA KIZAZI KIPYA (tuma)

tizneez

MAALUM KWA WASANII WA KIZAZI KIPYA (tuma)

Tanzania Urban Music Association (TUMA)Hiki ni chama kilichoanzishwa kwa malengo ya kuwasaidia wanamuziki wa kizazi kipya katika kutetea maslahi yao.

Chama kilianzishwa kutokana na mkutano mkubwa wa kwanza baina ya BASATA na wasanii wa kizazi kipya uliofanyika Diamond Jubilee Hall tarehe 2-11-2004.

Licha ya wasanii wa kizazi kipya kuwa wengi lakini katika uhalisia ni wasanii wachache waliojiunga katika miaka hiyo mpaka mwaka 2015, ingawa sasa mwaka 2016 ni wazi wameanza kujitokeza kujiunga kwa wingi ambapo katika mwaka huu tumeona wasanii kadhaa wakijiunga,kama msanii chipukizi Nikki wa Pili, , Jux, Barnaba,Kitale,Cyril, Ice Boy, Keisha, na hata mkongwe Mwana Fa na wengine wengi.

Chama hichi kina madhumuni mengi mazuri ya kumsaidia msanii wa kizazi kipya, kwani kila iitwapo leo muziki huu umeendelea kukua. Lakini kuna haki nyingi wanazopoteza wasanii wetu. Moja ya madhumuni makubwa ya chama ni,Kuwaunganisha wasanii wote wa muziki wa kizazi kipya chini ya chombo kimoja chenye jukumu la kueneza,kukuza na kuwaendeleza wasanii wa kizazi kipya, Kujenga uhusiano baina ya wasanii
Kuimarisha wajibu wa wasanii na kutangaza sanaa yetu nje ya nchi.
Kuwa kiungo na kutoa ushauri kwa wasanii kuhusu maendeleo na matatizo ya sanaa nchini.
Kusimamia na kutetea hakimiliki za wasanii wa kizazi kipya kwa kushirikiana na vyombo husika.Kupokea na kusimamia misaada,ruzuku na michango iliyotilewa na wafadhili kwa ajili ya chama, Kuwa chombo cha kutatua matatizo ya wasanii, Kusaidia uwezekano wa upatikanaji wa mikopo ya biashara ya muziki kwa wasanii, Kuwaweka wasanii katika chombo kimoja na kuwa na sauti ,Kusisitiza serikali kutengeneza mazingira mazuri ya sanaa katika kutetea na kupata maslahi yao.

Chama kina aina ya wanachama 3 ambao ni waanzilishi,walezi/wafadhili na wanachama wa kawaida (wasanii)

Kwa kujiunga na chama utakuwa na masharti unayopaswa uyafuate ambayo sio magumu kabisa,haki za mwanachama utazipata ikiwemo kupiga kura kuchagua viongozi,kugombea nafasi za uongozi ikiwa umekidhi vigezo na kushiriki katika shughuli za chama.

Chama kitakuwa na vyanzo vya mapato ambavyo vitatokana na ada za wananchama,ruzuku tika kwa baraza au taasisi mbalimbali za serikali na wafadhili ndani na nje ya nchi,miradi ya uchumi ya chama.

Chama kitakuwa na bodi ya wadhamini,kamati ya utendaji na walezi.

Imani ya chama ni kuwa sanaa ni muhimu sana katika ya jamii na ni kazi ya biashara.
Ukombozi wa wasanii kutokana na kutawaliwa kimawazo,kukandamizwa,kunyanyaswa na hasa kuonewa utapatikana kutokana na nguvu ya umoja wa wasanii wenyewe chini ya uongozi wa baraza chama na serikali.
Nguvu ya umoja wa wasanii italeta mapinduzi na maendeleo ya sanaa ndani na nje ya nchi.

Nimeandika baadhi ya mambo ambayo katika chama yataweza kuwa mwanga kwako wewe msanii wa kizazi kipya, katika hatua hii ambayo nina imani kwa kufuata taratibu na kujiunga utaweza kuwa na nafasi ya kufahamu mengine mengi ikiwamo kupata nakala yako ya katiba ili uweze kujua mengi zaidi na pia katika hili bado nafasi ipo ya kuendelea kuelimishana huku tukijiandaa na mkutano ambapo utatangazwa hapo baadae kwenye vyombo vya habari.

Umoja ni nguvu daima!Kama ni msanii wa kizazi kipya ni vyema kujiunga na chama chako cha TUMA

Kwa kifupi nawasilisha.
Asanteni.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez