Lord Eyez na utabiri wa anguko la muziki wake.

Lord Eyez na utabiri wa anguko la muziki wake.

Miaka kadhaa nyuma kundi la Nako 2 Nako lilikuwa moja kati ya makundi bora ya hiphop ambayo yamewahi kutokea katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Gnako, Ibra da Hustle, Bou Nako na Lord Eyez walikuwa ndio wasanii waliokuwa wameiweka Nako 2 Nako kwenye kilele cha muziki wa hiphop hapa Tanzania.

Licha ya kuwa wengi katika kundi hilo, ila uwezo wa Lord Eyez ulionekana zaidi katika midondoka na uandishi. Nyimbo kama Machafuko, Mchizi wangu, Bang, Ndio zetu, Iko wazi, Mizuka na nyingine nyingi hakika zilidhihirisha ubora wake na ukubwa wa kipaji chake.

Sanaa na Mapito hizi ni nyimbo za mwisho kutoa kutoka kwenye maktaba yake ya muziki. Licha ya kushirikisha wakali kama Joh Makini na Damian Soul lakini hazikuweza kufanya vyema kama ambavyo ilikuwa awali.

Wakati wakifanya vyema kama Nako 2 Nako hakika maneno ya kubebwa kama ilivyo sasa kwa upande wa Weusi yalikuwepo kutoka katika vijiwe vya hiphop. Ingawa katika uhalisia sikuwa nimezingatia bali niliamini katika vipaji vyao.

Moja ya maneno ambayo ukitazama sasa yalikuwa ni utabiri kama sio uhalisia kutoka kwa Lord Eyez ni yeye kusema “Yule atakaye kupandisha ndiye atakaye kushusha”, haya aliyasema katika wimbo wa hawatuwezi ambao walimshirikisha Enika. Ni wazi sasa ameshuka kimuziki hili halina kificho, maneno ya narudi kesho yamekua mengi kutoka kwenye kinywa chake na watu wake wa karibu (Weusi)

Nani alimpandisha Lord Eyez? na kwanini ameamua kumshusha kiasi hichi? Na kushuka kwake kimuziki Lord Eyez yeye aliyempandisha anafaidika na nini? lakini pia maneno juu ya matumizi ya madawa ya kulevya yamekuwepo, je ni madawa yanafanya azidi kushuka kimuziki?

Lakini katika swala la kupandishwa Fulani na Fulani limendelea kukua kila leo. Ila ni wakati wa msanii kujifunza kama sio kujua kama ukipandishwa ni vyema ukajitengenezea mizizi yenye maana ili washindwe kukushusha kama ilivyo kawaida yao.

Amka kifikra msanii.

Tunaamini katika kipaji cha Lord Eyez

 

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez