Lody Eyez chukua mfano wa Chid Benz ishi kwenye maneno ya Joh Makin.

Lody Eyez chukua mfano wa Chid Benz ishi kwenye maneno ya Joh Makin.

Ni wiki kadhaa zimepita tangu kwa msanii Lord Eyez kuachia ngoma yake ya ‘Hela Yangu’ ambapo ni wimbo wake wa kwanza tangu kuwa chini ya Baraka Da Prince.

Lord Eyez hapo awali alikuwa akiunda kundi la Nako 2 Nako ambapo lilikuwa na wakali kama G Nako,Bou Nako,Ibra Da Hustle, lakini kwasasa haijulikani hatma ya kundi hilo la Nako 2 Nako.

Weusi ndio kundi lake lililofuata ingawa katika mahojiano mengi msemaji wao Nikki wa Pili amekuwa akitoa msisitizo kuwa Weusi sio kundi bali ni Kampuni, licha ya mtaani kuendelea kujua kuwa ni kundi tu la Hiphop.

Weusi Kampuni/Kundi linaundwa na wasanii watano ambapo ni Nikki wa Pili, Gnako, Joh Makin,Bonta na Lord Eyez.

Lakini sasa katika taswira inaonyesha ni kama wapo watu watatu kwa muendeno wa kazi zao mara nyingi kusikika Gnako,Joh na Nikki wa pili.

Katika mahojiano ambayo alifanya Lord Eyez hivi karibuni katika kituo kimoja cha Radio alisema “Siku zote makundi yanavunjika kwa vitu vitatu, Ubinafsi, Mminyo, na Kubaniana. Kanuni za Weusi ilikuwa ni mgawanyo asilimia 20 kwa wasiofanya kazi, lakini sasa kuna Weusi ya River Camp”

Maneno hayo aliyasema wakati akitambulisha wimbo wake mpya. Kumekuwepo kwa hoja nyingi katika vijiwe vya wapenda muziki juu ya meneno hayo ambayo inaoenekana kama ni kuwachafua Weusi kwa mujibu wa wapenda muziki.

‘’Jambo jema ni kukumbushana yaliyo mema”Mwaka 2006-2010 ni wakati wa Nako 2 Nako walikuwa moto hakuna aliyepinga ubora wao kwa wakati huo.Ila malalamiko ya kubaniwa na ubaguzi yalikuwepo pia kutoka kwa Ibra Da Hustle na wakati huo Lord Eyez ndiye kiongozi wa kundi hilo la Nako 2 Nako.

Malalamiko pekee hayajawahi kumsaidia Ibra Da hustle bali kutumbukia shimoni mpaka leo. Njia ya pekee ya kuepuka mminyo,ubinafsi na kubaniana ni kufanya kazi za upekee Zaidi bila kuwaza kulalamika mbele ya media.

Mwaka 2010 Joh Makini alitoa  wimbo wa ‘Ufalme’ ambapo katika wimbo huo alizungumza mengi, ila moja wapo ambalo linaendelea kuwagusa wasanii wengi ni Joh kusema “Uwanja bado ni mpana kuna mengi ya kufanya, saka maushindi hata kwa njia za panya.

Kiuhalisia uwanja wa muziki wa kizazi kipya ni mpana mno, kila msanii anaweza kusaka ushindi kwa njia zake ambazo anaamini zitamfanya apate kipato cha kukidhi mahitaji yake na familia yake.

Wakati Chid Benz anarudi na wimbo wake alitoa malalamiko mengi juu ya wasanii wengi akiwemo Joh Makin, na alisahau kabisa kuwa uwanja huu wa muziki wa kizazi kipya ni mpana. Chid Benz alisahau kabisa kuzungumzia wimbo wake bali kusema Joh anabebwa, mashabiki wa sasa sio wa zamani wengi wa sasa wanaamini mara wanaposikia kazi nzuri tu.

Lord Eyez anapaswa kujifunze kwa Chid Benz maana alivyorudi ndani ya wiki ya kwanza alipotea shauri ya muda mwingi kutoa malalamiko na sio kutambulisha kazi na kueleza mipango mipya.

Hivyo umakini katika kinywa chake unahitajika, vinginevyo itakuwa Kurudi ghafla  na kupotea ghafla kwa lord Eyez.

Malalamiko hayawezi kusaidia kuendelea kimuziki, bali kazi nzuri kwa muda mzuri.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

 

Mwisho.