LADY JAYDEE AANZA MWAKA NA SAUTI SOUL

JD_65

Give me love ni wimbo wake komando Jide ulioachiwa mwaka jana ambao alifanya na Mazet Uhuru nchini Afrika kusini.Jide ambaye ni mkongwe na msanii pekee wa kike aliyeweza kudumu kwa miaka yote tangu aanze muziki licha kuwepo kwa changamoto nyingi katika mziki hasa katika upande wao wa wasanii wa kike.

Lady Jaydee kupitia mtandao wa picha Instagram alipost picha akiwa na mmoja kati ya wasanii wanaunda kundi la Sauti Soul ambalo ni kundi linalofanya vizuri katika ramani ya Afrika na nje pia.Picha hiyo ambayo imeonyesha wakiwa studio inaonyesha dhahiri wakiwa wakirekodi wimbo.Licha ya hivyo pia Jide hakusita kumpost meneja wake ambaye ni Seven Mosha ambaye pia ndiye meneja anayemmeneji msanii Ally Kiba.

jid