Kwenye Jibebe Tekno, Davido, na Diamond Platnumz hakika Dully Sykes atawabeba.

Kwenye Jibebe Tekno, Davido, na Diamond Platnumz hakika Dully Sykes atawabeba.

Jibebe ni wimbo wa Wcb ambao Mbosso, Lava Lava na Diamond wameweza kuleta ukamilisho wa wimbo huu. Na ni wazi wimbo umeweza kwenda kwa upana katika nyakati fupi mno.

Na tumeona kwa upana ambao Diamond akiweka wazi katika mtandao wa picha ‘Instagram’ juu ujio wa rudio wa wimbo huo. Ambapo Davido, Tekno na Dully Sykes watakutana katika wimbo huu wa Jibebe.

Na wajuzi hawaachi kunena hadharani yakuwa Dully Sykes atawabeba wote katika wimbo huu, maana upana wa Dully katika uimbaji ni mpana kuliko ambao atakuwa nao katika wimbo mmoja.

Na ni jambo jema kwa Diamond kuweza kutafakari katika kutanisho la wasanii hao hakika itakuwa Jibebe yenye uhakika zaidi. Lakini ni faida kubwa kwa Dully kuendelea kwenda sawa na vijana wenye upya na upana wa soko.

 

#TuzungumzeMuziki