“KWELI HAKUNA JIPYA CHINI YA JUA“? DIAMOND PLATNUMZ

diamond-1940x720

“KWELI HAKUNA JIPYA CHINI YA JUA? “ DIAMOND PLATNUMZ

Kumekuwa na maneno mengi tangu kutoka kwa nyimbo ya Make me sing ya mkali Diamond Platnumz akiwa na AKA tokea South Afrika,lakini maneno hayo yamekuja baada ya watu kutazama video hiyo.

Siku hizi imekuwa kawaida kwa mashabiki kutumia mida mwingi kukosoa kuliko kupongeza, hii hainishangazi hata kidogo maana team zao zilizopo mitandaoni hususani mtandao wa picha ndizo zenye kukosoa kuliko hata waliosomea au wenye uwezo zaidi katika kuchambua au kufanya hizo video.

Diamond hakusita kuweka wazi kile anachokiona ni sawa kwake ambapo alisema” watu wanashindwa kuelewa kila kitu ambacho kinafanyika sasa hivi kwenye muziki kuanzia video,mashairi na vyote tayari vilishafanyaika vyote. Na hata vingine vilishaimbwa yani ni kama vinafanyika tena kwa marudio lakini kila mtu anarudia kwa namna yake”

Je kweli hakuna jipya chini ya jua?

Tupe comment yako hapa

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

 

 

Source Sam Misago