Kwanini wasanii wengi hawawekezi nje ya muziki?

Kwanini wasanii wengi hawawekezi  nje ya muziki?

Muziki wa kizazi kipya umeendelea kukua siku baada ya siku, ila moja ya changamoto ambayo inaowakumba wasanii ni kuto kuwekeza nje ya muziki.

Swala la kuwekeza nje ya muziki ni jambo jema, maana hata kama muziki utakuacha basi utaendeleza maisha mengine kwa upande wa pili wa uwekezaji nje ya muziki.

Ni ukweli usiopingika wasanii wengi wamekuwa wakiamini katika muziki tu bila hata kuwaza kuwa muziki wake unaweza kuwa ni mtaji wa kufanya biashara nyingine. Maana katika ramani ya dunia hakuna msanii ambaye ataweza kufanya vyema milele, hivyo wasanii wetu wanaandaa kesho zao za aina gani?

Leo hii nimezungumza na O Ten ambaye ni moja kati ya wasanii waliowahi kufanya vyema katika ramani ya muziki wa kizazi kipya, wimbo kama Nicheki, Sifa kumi za demu, Voice mail, Mimi na nyingine nyingi zilifanya aweze kukubalika na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.

Lakini moja ya mambo aliyosema ni “Nipo kimya najichanga ili niweze kutoa video kali kama ambazo wanatoa wengine”

Je kutoa video kali ni mpaka ujichange? Ni wazi inaonyesha hakuwekeza nje ya muziki, hivyo show chache anazopata sasa ni lazima atumie muda mrefu kujichanga ili aweze kutoa video hizo zenye kiwango cha kimataifa.

O Ten ni mmoja kati ya wasanii ambao wanajipanga kurudi katika game na hata kufanya hizo video za kiwango cha kimataifa, ila wapo wasanii wengi ambao wanashindwa kurudi maana hawana pesa ya kukimbizana na upepo wa sasa kwenye muziki.

Muda umefika kufikiri nje ya uwanja kuweza kuwekeza katika biashara nyingine sio muziki pekee. Maana uwekezaji nje ya muziki pia utafanya uweze kurudi katika muziki mara tu unapohitaji kwani hautakuwa na mkwamo wa kifedha.

Amka msanii Muda ndio huu.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez