Kwa mara ya kwanza Dully Sykes na Juma Nature kufanya wimbo.

Kwa mara ya kwanza Dully Sykes na Juma Nature kufanya wimbo.

Kila mmoja anajua uwezo wa wasanii hawa katika uwanja wa muziki wa bongo fleva.

Ni ngumu kuwalinganisha lakini kila mmoja anajua kurap na kuimba na hiyo ni katika nyimbo kwenye album zao tofauti.

Lakini katika maisha yao yote ya muziki hawakuwahi kufanya wimbo wowote pamoja, na ni wasanii ambao hawajawahi kuwa na tofauti yoyote ile.

Na mwaka huu kwa mara ya kwanza watakutana katika wimbo mmoja ambapo wimbo huo umetayarishwa na Mr T Touch chini ya Touch Sound.

Na kwa mujibu wa Rich One ambaye ni mtu wa karibu zaidi wa Juma Nature amethibitisha na kusema “Ngoma iko tayari na tunasubiri muda sahihi tu itoke, na huu ni wimbo wa kwanza kuwakutanisha Juma Nature na Dully”

#TuzungumzeMuziki