KUTENGULIWA KWA NAPE NAUYE KWAIBUA HISIA TOFAUTI

Mapema hii leo, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi waliyekuwa  waziri wa Habari,  Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nauye kama waziri wa habari wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia habari yake kwa vyombo vya habari kama inavyoonekana hapo chini.

Aidha kutenguliwa kwa Nape Nauye kumeibua hisia mbali mbali katika mitandao ya kijamii. Watu wengi wakilihusisha hili kama adhabu ya yeye akiwa kama waziri mwenye dhamana kuunda tume maalumu ya kuchunguza mkasa uliofanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam (Paul Makonda) katika kituo cha habari cha Clouds mwishoni mwa juma lililopita.

Baadhi ya wadau pamoja na wasanii wamekuwa na hisia tofauti katika hili, na hawakusita kuweka hisia zao hadharani kupita kurasa zao za mitandao ya kijamii. Zifuatavyo ni baadhi ya Posts za watu waliogushwa na tukio hili.

Hayo ni baadhi tu ya maoni ya watu ambao Tizneez Tapo tumekuwekea lakini kila kundi linamono yake katika hili.

Nafasi iliyoachwa na Mhe Nape Nauye itachukuliwa na Mhe. Harrison George Mwakyembe ambaye ataapishwa kesho tarehe 24 – Machi – 2017.

Tizneez Tapo tunatoa pole kwa Mhe. Nape Nauye kwa kupoteza kiti chake cha uwaziri katika Baraza la Mawaziri akiwa kama mwakilishi wetu sisi wana habari na wana sanaa, utamaduni na burudani. Lakini pia tunapenda kumpongeza Mhe. Harrison Mwakyembe kwa uteuzi kwa kuchaguliwa kuihudumia wizari hii.

Ukiwa kama mtanzania na mzalendo, wewe una maoni au mtazamo gani katika hili? Unaweza kutoa maoni yako kwa kucomment hapo chini. Karibu…