‘Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzie, wote watatumbukia shimoni’ TID na KR Muller

“Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzie,  wote watatumbukia shimoni” TID na KR Muller

Zeze ni wimbo uliotambulisha Tid kwenye ramani ya muziki ya kizazi kipya, lakini pia Yamenikuta ni wimbo ambao ulitambulisha Kr Muller akiwa na kundi lake la GWM kabla ya Wachuja Nafaka, Wanaume Family na baadae Wanaume Halisi.

Ni mwanzoni mwa mwaka 2016 ambapo TID Mnyama alimtambulisha KR Muller kuwa chini ya Label yake ya Rader Entertainment, ambapo katika moja ya mahojiano ya kipindi cha Radio TID alisema “Nimechukua KR Muller kuwa chini ya Rader maana nimeona nguvu yake wakati tukienda kwenye kampeni Mtwara.

Huwezi amini kila tulipokuwa tunapita watu walikuwa wakishangilia hivyo nimeona ni jinsi gani watu wanampenda nikaona ni vyema nimchukue nifanye nae kazi”

Tangu Tid kutangaza kumchukua Kr Muller ni miezi 8 imepIta sasa na hakuna kazi ambayo imewahi kusikika kutoka kwa KR Muller, isipokuwa malumbano kati ya Juma Nature na Tid juu ya Kr Muller.

Lakini katika uhalisia ni wazi TID sasa hizi hafanyi vizuri kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya, licha ya kutoa kibao chake cha Confidance ambacho alimshirikisha Joh Makini na Dully Sykes, ila kibao hicho hakijafanya vizuri.

KR na TID wote hawafanyi vizuri katika ramani ya muziki wa kizazi hivyo ni ngumu mmoja kutaka kumtoa mwenzake. Kuna msemo unasema Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzie wote watatumbukia shimoni”

Hili naliona katika maisha ya muziki wa TID na KR Muller, TID anataka kumuongoza KR Muller wakati wote hawafanyi vyema kwenye muziki. Hivyo watawezaje kufanya vyema? Au TID atawezaje kumfanya KR Muller afanye vizuri kwenye muziki ilihali yeye mwenyewe hajaweza kujirudisha na kutawala kwenye muziki kama ilivyokuwa zamani.

Je wewe una mtazamo gani katika hili? Tupe maoni yako chini hapa

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez