“Kilichofanywa na Belle na G nako ni remix ya wimbo wangu” Tox Star

“Kilichofanywa na Belle na G nako ni remix ya wimbo wangu” Tox Star.

Tox Star sio jina jina katika uwanja wa muziki wa kizazi, licha ya sasa kutofanya vyema ila amekuwa akiendelea na kazi zake za kimuziki.

Wimbo wa Pretty Girl akiwa na Ali Kiba ni wimbo wake ambao ulimtambulisha vyema miaka kadhaa nyuma.

Mapema kupitia mtandao wa picha Instagram msanii huyo ameandika “Muziki ni burudani. Napenda sana nikikutana na changamoto wakati nikiendelea na kazi yangu ya muziki maana inanikuza kiutunzi hata kuwa na mbinu mpya ili nifanye mziki mzuri.

Nimegundua ninachofanya au muziki ninaoimba kumbe unafika sehemu Fulani na watu wanaelewa hata wengine wakiwa ni Wanamuziki wenzangu.
Kiukweli nime appreciate kilichofanywa humu kiupande mwingine naona kama ni remix ya wimbo wangu OLE ft SESEME @spincesesemee
Acha tuburudikeni na Muziki wetu…One love
#MZIKI_SIO_VITA

Tox Star aliandika hayo ambayo ni wazi yameenda kwa Belle 9  pamoja na Gnako na hapa chini ameweka wimbo huo.

Sikiliza hapa chini

 

 

 

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa