Kauli ya Nikki wa Pili ina maana kubwa na wengine muitafakari vyema. (Media)

Kauli ya Nikki wa Pili ina maana kubwa na wengine muitafakari vyema. (Media)

Nikki wa pili ni moja kati ya wasanii walio chini ya mwamvuli wa hiphop ambaye Quality time ni wimbo wake ambao unafanya vizuri kwenye media kwa sasa.

Nikki wa pili  nyakati zote husimama katika kauli zenye kuleta tija na maana kwa jamii ya muziki lakini hata nje ya muziki pia.

#TuzungumzeMuziki ni maisha yetu Tizneez kwa maana ya wakati wote tunazungumza muziki tu na sio jambo la kiki. Lakini media nyingi kuzungumza muziki ni jambo baya bali zuri ni kuzungumza kiki.

Katika ile kauli ya Nikki wa Pili ya kuandika katika mtandao wa picha Instagram “Kwa upande wangu mimi kama mimi mwaka 2017 sijasikia wimbo wa kuimba mkali kama huu”

Ni wazi wimbo huu wa Protocol ni wimbo bora 2017 kwa kipimo  cha mashairi,mdundo na uimbaji wa Rama Dee. Lakini Media zetu hazina muda wa kuzungumza muziki Zaidi ya kiki.

Ni vyema kubadilika na kutazama muziki ambao utaweza kufanya tuendelee mbele Zaidi kuliko kiki ambazo haziwezi kusaidia kuinua wala kujenga muziki wetu.

#TuzungumzeMuziki

 

 

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa