Kauli ya Fid Q inagusa uhalisia wa Chege na Madee.

Kauli ya Fid Q inagusa uhalisia wa Chege na Madee.

Fid Q ni  moja kati ya wasanii wa hiphop bora ambao tumebahatika kuwa nao katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Mtaji wa mistari ndio kitu pekee kilichompa mashabiki wengi wa muziki wa hiphop. Ila pia aina ya flow zake ni kitu kingine ambacho kimezidi kumuweka tofauti na wasanii wengine.

Hoja za muziki wa hiphop sio biashara zilitawala miaka kadhaa nyuma, lakini pia bado wapiga miluzi wameendelea kusema hoja hiyo ambayo kiundani ni hoja dhaifu. Hoja hiyo ilinifanya kuandika Makala ya Hakuna muziki usiokuwa biashara na hapo niliezea kwa mapana zaidi juu ya aina zote za muziki na mifano iliyo hai.

Wakati wa kuanza muziki kati ya Madee na Chege wote walikuwa ni wasanii ambao wapo chini ya kivuli cha hiphop.

Miaka michache baadae Madee alitoa wimbo wake wa Hiphop haiuzi, hoja hii ilipata majibu kutoka kwa wadau wa hiphop na hata wasanii husika. Na miaka kadhaa baadae Madee akaanza kufanya muziki anaofanya sasa ambao sijui ni aina gani ya muziki, bali tumemsikia akiwa anaimba.

Ukiitizama hoja ya muziki wa hiphop sio biashara kwa jicho la tatu utagundua hoja  ya Madee haikuwa na maana bali ni hoja ya mawazo madogo “Hakuna muziki usiokuwa biashara

“Mimi” ni wimbo wa Geez Mabovu ambao alimshirikisha Jay Mo, Chid Benz, na Fid Q.

Fid Q alikuwa ni msanii aliyefanya verse ya mwisho, na katika verse hiyo hakusita kuweka uhalisia wa muziki vile ambavyo unakwenda. Ambapo katika verse hiyo amesikika akichana “watoto wanataka kurap mabosi wanataka waimbe”

Kauli hii inagusa uhalisia wa maisha ya kimuziki kwa upande wa Chege na Madee, ambao sasa wamegeuka kuwa waimbaji na hata kwenye matumbuizo yao wanapanda na wacheza shoo. Ambapo kila mpenzi wa muziki anaamini mabosi zao katika Babu Tale na Mkubwa Fella ndio wamewaamulia wasanii kufanya wanachofanya.

Lakini kwanini mabosi hawataki msanii afanye muziki wa hiphop bali aina nyingine? Je hawaoni kumpangia msanii cha kufanya ni kuweka mipaka kwenye kipaji chake?

Kauli hii ya inaendelea kuishi mpaka sasa kwa wasanii wengine. Tumeona Rayavany na Dogo Janja nao wamekuwa waimbaji wazuri kabisa, ingawa naamini wangefanya vizuri zaidi ya pale kama wangefanya kile ambacho wanapenda zaidi.

Ni vyema kujua namna ya biashara ya muziki, Hakuna muziki usiokuwa biashara.

Je ni sawa kwa hawa ambao wanajiita mameneja kumpangia msanii cha kufanya?

Tupe maoni yako hapa chini

Lakini pia tufuate katika mitandao yetu ya kijamii hapo chini.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez