Katika list ya wasanii 5 wanaohitajika Kigoma Harmorapa aongoza.

Katika list ya wasanii 5 wanaohitajika Kigoma Harmorapa aongoza.

Ni tangu tarehe 2/3/2017 Team Tizneez iliweza kufika Kigoma katika mambo mengi yanayohusu muziki wa kizazi kipya.

Ikumbukwe www.tizneez.com ni mtandao unaojihusisha na muziki wa kizazi kipya tu, yani Bongo Fleva na Hiphop.

Kwa kuwa tupo kwaajili ya muziki wa kizazi kipya na tunawatakia yaliyomema wasanii wote hivyo haitupi shida katika kuwafungua wasanii mahala ambapo mashabiki wao wanauhitaji nao zaidi.

Utafiti huu ambao umefanywa kwa siku tatu kuanzia siku ya Jumatatu ya tarehe 3/3/2017 mpaka siku ya tarehe 5/3/2017.Ambapo pia utafiti huu ulihusisha maeneo ya Kigoma mjini tu.

Utafiti huu ulifanyika kwa njia ya kuuliza wadau wa muziki kuanzia madj, mapromota lakini pia shabiki ambaye ndiye mteja mkuu hapa Mjini Kigoma.

Na katika utafiti huu tulilenga kupata majina 5 tu ya wasanii ambao wanahitajika Zaidi hapa Kigoma Mjini.

Wasanii ambao waliweza kupatikana katika kundi la wasanii 5 ambao tulikuwa tunahitaji ni

. Harmorappa

. Weusi

. Darassa

. Ali Kiba

. Diamond Platnumz

Ziada ni msanii Nay wa Mitego pamoja na Navy Kenzo

Hayo ndiyo majina ya wasanii 5 ambao wanahitajika katika Mkoa wa Kigoma, na jambo hili la kuwahabarisha wasanii mahala wanapohitajika ni jambo endelevu.

Wasanii tajwa ni vyema mkatafakari neno hili “ Tumia wakati  kwa wakati kwa kufanya la wakati huenda ikafika wakati ukakosa wakati wakufanya la wakati, kwani wakati ukuta”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa