Katibu wa Basata azungumzia sakata la Nay wa Mitego asema amevunja sheria zaidi ya mbili.

3b7949c7aa633a847e5dd6108eee8a63

Katibu wa Basata azungumzia sakata la Nay wa Mitego asema amevunja sheria zaidi ya mbili.

Sakata la Nay wa mitego kufungiwa kwa wimbo wake wa “Pale kati patamu” limeendelea kuchukua sura nyingine siku baada ya siku.

Wakati katika mahojiano mengi aliyokuwa anafanya msanii Nay amekuwa akisema kuwa hajapata barua ya kufungiwa kwa wimbo wake wa “Pale kati patamu”

Katibu wa Basata hakusita kuweka wazi ambapo alisema “Ni kweli tumefungia wimbo huo kama ambavyo tulifungia wimbo wa shika adabu yako. Kufungia nyimbo si lazima tukupe barua au tukuite kwaiyo wewe ambaye unatumia ule wimbo uliofungiwa ni kosa. Kwa kufungia wimbo huu tumefanya taratibu na kanuni, lakini pale inapoingia kwenye mitandao ujue kabisa kuna sheria nyingine.

Hivyo hakuvunja sheria moja amevunja sheria ya basata amevunja sheria ya mitandao tena ya juzi tu hapa 2015. Hivyo katika kosa moja amevunja sheria zaidi ya mbili. Pia sheria ya content za kuweka mitandaoni amevunja.

Pia anaposema hajawapewa barua kufungia kazi si lazima upewe barua, ni hakika barua amepata na ndani ya wiki hii atakuja hapa Basata. Kwasasa hivi alipofikia adhabu hii inaweza ikatosha au isitoshe, ila pia wanajidanganya kwa kusema wanapata kiki.

Mfano kama unaendesha gari na huna leseni waweza kuendesha miaka 10 hivyo siku ya kukamatwa unaweza ukajutia miaka hiyo. Lakini pia hajajisajili Basata lakini juzi alipokuja amechukua fomu.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez