‘Kama hujui unapotoka hakika hutajua unapoenda’ Black Chatta

‘Kama hujui unapotoka hakika hutajua unapoenda’ Black Chatta

Mistari ni wimbo wake ambao ulimtambulisha vyema katika ramani ya muziki wa kizazi kipya. Black Chata pia ni mdogo wa damu wa msanii mkongwe Prof Jay ambaye sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi katika Mkoa wa Morogoro.

Huwezi kutaja nyimbo bora za wakati wote katika ramani ya muziki wa kizazi kipya bila kutaja wimbo wa Usipime kutoka kwa mkali Black Chatta.

Blach Chatta ni wimbo wake ambao ulitoka mwaka 2009, ambao wimbo huu uliweza kumbadilisha jina kutoka Black Rhino mpaka kuitwa Black Chata. Hakika mafanikio ya wimbo huu yalikuwa makubwa mno, maana wimbo huu uliweza kuwa moja kati ya nyimbo pekee zilizoweza kuchaguliwa katika tuzo kubwa za Channel O mwaka 2009.

Wimbo huu ulikuwa katika Kipengere cha Video bora ya mwaka, na video ya wimbo huu ilifanywa na Adam Juma wa Next level, lakini wakati huo kampuni yake ikiitwa Visual Lab.

Hizi ni moja kati ya movement chache zilizosaidi muziki kufika hapa ulipo. Kama hujui wapi umetoka basi hujui wapi unakwenda.

Team Tizneez tunatambua na kuheshimu mchango wako katika muziki wa kizazi kipya.

Tumethrobck na Black Chatta hebu tuambie ni ngoma gani unaipenda zaidi kutoka kwake

Tuambie hapo chini.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez