KALAMU YA NIKK WA PILI

Nikki-wa-Pili_2

Msanii chipukizi Nikki wa Pili, ambaye ni mwanazuoni mapema leo ametoa mtazamo wake juu ya elimu ambapo ameandika hayo kupitia mtandao wa picha Instagram.

Nikki amendika “KALAMU YA NIKKWAPILI
JE KUFELI AU KUFAULU…KWA MWANAFUNZI HAKUTOKANI NA UWEZO WA KIAKILI ?
Tofauti kubwa kati ya mwanafunzi anaye faulu na anaye feli pia hutokana na msukumo wa kusoma alio nao mwanafunzi husika, anaye faulu anakuwa na msukumo mkubwa wa kusoma na anaye feli anakuwa na msukumo mdogo.
Ili kuwa na msukumo mkubwa lazima tuwaoneshe wanafunzi..namna mchakato wa kusoma ulivyo sexy ili tutongoze hisia zao nakuwapa msukumo wa kuupenda mchakato wa.kusoma na kujifunza
NGOJA nieleze kidogo kwa mifano the baeuty(uzuri au sexiness) ya mchakato wa kusoma (na maanisha mchakato the process sio masomo yenyewe). Nianze na “Kukariri”
kama sehemu kubwa ya mchakato wa kusoma Tanzania.
mwanafunzi Anapokuwa ana kariri masomo yake…pia kuna uwezo anaujenga ndani yake(kuna utamu wake)….mfano mimi kukariri kunaniwezesha leo nakariri nyimbo zaidi ya ishirini kichwani, naweza kuandika wimbo kichwani bila peni wala daftari, kukariri kutakusaidia kuja kuwa bingwa wa kutowa hotuba (speech) bila kusoma, kutakuwezesha kufanya presentation nakadhalika….mwanafunzi anapo kariri atambue pia anajijenga akitambua hivyo hata chukia hilo zoezi, “KUANDIKA NOTES”
Unapoandika notes wakati mwalimu anafundisha…ndio kujifunza kuja kuwa mwandishi wa habari, msaidizi wa raisi ama waziri, ama msaidizi wa boss, ama kuwa mtafiti….mwanafunzi akijuwa hili atapenda zaidi na zaidi kuwa anaandika notes,
“KUSOMA KITABU”
Unaposoma kitabu….haijalishi unasoma nini…unajenga uwezo wa ku focus na kuko concentrate …hii ni skills muhimu sana maishani, inahitajika kwenye biashara, jeshini, michezoni, sanaa,dini, kwenye mahusiano nakadhalika
“KUFANYA assignment”
Mfano Unapo solve hisabati, fizikia, bookkeeping..una jenga uwezo wa kutatuwa matatizo..na kulingana na world economic forum hii ndio skills namba moja inayohitajika duniani. “Kusikiliza mwalimu” anapofundisha, kuwa na uwezo wa kuskiliza hii pia ni skills namba 9 inayohitajika duniani,ukiweza kuskiliza kwa makini unaweza kuwa mbunifu wa masoko, mboresha huduma, mtunzi mzuri, mshauri au kiongozi”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez