KALA JEREMIAH HAKUNA KAMA PROF JAY

kala
Msanii wa muziki wa hip hop Kala Jeremiah ambaye pia amewahi kuchukua tuzo ya msanii bora wa hip hop pamoja na nyimbo bora ya hip hop dear god mwaka 2013 katika tuzo za KTMA.Kala kwwasasa anafanya vizuri na nyimbo yake aya inchi ya ahadi aliyomshirikisha mkali Roma.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Kala aliandika:Miaka itaenda miaka itarudi wasanii watakuja wasanii wataondoka hakika hawezi kutokea Prof Jay mwingine wala wa kufanana nae.Heshima yake itabaki milele,alivyowahi kufanya si vya kawaida amefanya kazi kubwa sana kwanza alibadilisha muziki na kuufanya kukubalika na watu wote.Akaondoa ile dhana ya muziki ni uhuni akatunga tungo za kumshawishi kila mtu akubali akatae.Na sasa imani yangu ni kwenye swala lake la kugombea ubunge Mikumi ni kubwa sana naamini yale mapinduzi aliyoyaleta kwenye muziki atayaleta pia bungeni.Kwa wana mikumi wote muda ukifika mpeni kura ya ndio maaana anaweza.