KALA JEREMIAH CHAGUA MTU SIO CHAMA

eatv_hot-mix_kala-jeremiah-27-3-131
Nchi ya ahadi ni nyimbo yake inayofanya vizuri wakati huu katika media mbalimbali,Kala Jeremiah ni moja kati ya wasanii wa hip hop wanaofuatilia sana swala la siasa.Licha ya Kala kufanya nyimbo za kuhamisha na kuelimisha katika nyimbo zake,kwasasa ameamua kuwaasa watanzania juu ya uchaguzi unaokuja hivi karibuni.
Kala Jeremiah alisema kuna umuhimu sana wa watu kuamka na kuchagua kiongozi bora na sio chama alichopo,yani watu wachague mtu sio chama.