K WA MAUJANJA WATANZANIA WAMEBADILIKA SIJUI WAMEPEWA NINI

maxresdefault
K maujanaja ni msanii wa hip hop tokea kundi la Maujanja saplaya lenye maskani yake Mwenge Dar es salaam.Team tizneez inaendelea kukuletea maoni wanayotoa wasanii mbalimbali kueleka uchaguzi mkuu october 25,Na hapa ni zamu ya K wa Maujanja Saplaya
Kupitia ukurasa wake wa facebook ameandika “Kiukweli watanzania sasa hivi wanabadilika sana halafu wana maujanja mengi sana, pia wasomi ni wengi sana, sasa ni hivi ukijifanya una akili sana nao wanakuja na maswali mengi halafu wanakujadili, kifupi hawa watu sidhani unaweza kuwasomesha tena kwa sasa uelewa ni mkubwa sana miongoni mwa watanzania. Miaka mitano iliyopita sio kama sasa watanzania sijui wamepewa nini, sasa wanasiasa muangalie sana wangine mnajichoresha ni bora tu kukukaa kimya au mfanye kampeini za ukweli kama umepewa hela fikiria kwanza cha kuongea mwingine anakuja kuongea unamjua tu kisha pewa hela na pia angalieni sana unaweza kumpa mtu rushwa akala hela na asikuchague chunga sana”
K-wa-MAPCHA
Unaweza kuwa rafiki yetu facebook.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez