Juzi na Jana ya Rama Dee na Clouds Media Group, si kama leo

Katika kudhihirisha usahihi wa kauli ya “Juzi na Jana si kama leo” iliyonenwa na wahenga. Msanii nguli wa miondoko ya RnB ambaye tulio wengi tunamfahamu kama Rama Dee na Clouds Media Group. Wameamua kuwa waungwana sambamba kama ambavyo wahenga walivyonena kuwa ‘ada ya muungwana ni kitendo’. Kwa kuamua kufunika kombe china na kwa hiari yao kuamua kutafuta suluhu na kumaliza mgogoro wao uliodumu kwa muda mrefu.


Mapema leo Rama Dee ametuacha vinywa wazi tulio wengi baada ya kusambaza picha iliyokuwa ikihabarisha umma juu ya mahojiano yake katika kipindi maarufu cha XXL kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds FM kila siku za juma. Rama Dee atafanya mahojiano katika XXL ikiwa ni muendelezo wa safari yake ya kutambulisha wimbo wake mpya unaofahamika kwa jina la NIBEBE.
Hakika hakuna marefu yasiyo ncha, Rama Dee na Clouds Media Group wamealidhihirisha hilo. Hatuna budi kuwapa Heko kwa maamuzi ya busara ambayo yamewaweka pamoja na kurejesha hari ya kuendelea kufanya kazi pamoja katika kusukuma gurudumu la Muziki wetu.
Yaliyopita si ndwele, hatuna budi kuganga yajajo. Na kuzifukia tofauti zote zilizokuwepo baina ya makundi haya mawili sisi kama mashabiki na wapenzi muziki.
#ZimaKikiWashaMuziki