JOHN DILINGA MADJ WANA TAMAA NA WIVU

index

Dj JD ameyasema hayo katika mahojiano na kipindi cha PlanetBongo kinachorushwa na East Africa Radio na kusema tatizo hilo lipo sana miongoni mwa DJs wa siku hizi na hutokana na kutopenda maendeleo ya mtu.

“Tatizo mi nafikiri inawezekana ikawa within damu zetu za kiafrika unajua sisi waafrika kila mtu hapendi mwenzake afanikiwe, kila mtu anataka afanikiwe yeye tu pasipo kuelewa kuwa anapofanikiwa mtu ambaye anamfahamu kwa namna moja au nyingine ujue na wewe utafanikiwa, ni ubabaikaji na ulambaji wa maDJ ambao wanababaikia wasanii wa bongo fleva, dj hutakiwi kwanza kuwa na team”, amesema Dj JD.

Pamoja na hayo akitolea mfano yeye mwenyewe katika utendaji wake, JD amesema wakati yeye anaaza ‘kuipromote’ bongo fleva, hakuwa akiwafahamu baadhi ya wasanii, na kwamba alipiga kazi za msanii yeyotebila kujali, ili mradi awe amefanya kazi nzuri

“Mimi katika historia yangu ya kufanya industry kama ni kupiga bongo fleva mimi nimepromote bongo fleva kupita maelezo, lakini wakati mi napiga bongo fleva napromote bongo fleva nilikuwa sijui msanii gani ni nani na timu gani ni nani kwanza nilikuwa napiga nyimbo za wasanii wengine sijawahi kuwaona wala kuwasikia, as longer as umefanya kazi nzuri”, alisema DJ JD.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

Source EA Radio en www.eatv.tv