Joh Makin ni mtu wa vitendo sio maneno.

Joh Makin ni mtu wa vitendo sio maneno.

Huwezi kutaja marapa bora  waliopo katika kivuli cha hiphop bila kutaja jina la Joh Makin.

Waya ni wimbo wake ambao bado unafanya vyema lakini pia Madaraka ya kulevya ni wimbo kutoka kwenye kampuni yao ya Weusi unaofanya vyema Zaidi kwa sasa.

Ni ukweli usiopingika tangu kufahamika kwa Joh Makin kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya amekuwa akipanda juu kimuziki kila leo. Joh sio mtu wa kusema kazi hii ndio hufuata au hii hapana, daima ni mkimya na mara zote huongea mara baada ya kazi kutoka.

Mapema leo katika mtandao wa picha Instagram msanii kutoka Nigeria Davido aliweka posti ambayo ameandika “Back to work !! On set 📽 shoot @johmakinitz ft Davido ….. TZ 🇹🇿 x NAIJA 🇳🇬.

Hii ni hatua kubwa katika muziki wa rap hapa Tanzania, wasanii rap wanapaswa kuamka na kufanya collabo nyingi ili kuendeleza muziki wetu mbele, joh peke yake hatoshi bali uwingi wa wasanii wetu katika collabo za nje unahitajika.

 

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa