“Joh Makin Ana kila sababu ya kuwaita baadhi ya mashabiki maandazi”

“Joh Makin Ana kila sababu ya kuwaita baadhi ya mashabiki maandazi”

Kelele za mashabiki juu ya wasanii katika mambo mengi ni nyingi mno. Lakini kelele zao mara nyingi ni katika mlengo wa kukatisha tamaa na vitu ambavyo havijengi.

Moja ya hoja ambazo walipiga kelele juu ya Joh Makini ni Davido kutokupost kava au clip fupi mara baada ya video ya wimbo huo kutoka.

Lakini mashabiki hawa wanasahau juu ya Davido ndiye aliyekuwa wa kwanza kuomba callabo lakini kuwa wa kwanza kuandika Twitter kuwa collabo yake na Joh inakuja. Ila wanasahau sauti ya Davido katika wimbo huo ni muhimu Zaidi kuliko posti moja ya Instagram.

Ila katika ufanyaji wa video nchini Afrika ya Kusini Davido alikuwa mtu wa kwanza kuposti tena wakiwa location.

Hivyo katika utoaji wa wimbo alichelewa kuposti na mashabiki walionekana kuogea kupita kiasi. Jambo ambalo linaonyesha ni wazi ni mashabiki wa juu juu wasiojua lolote kwenye muziki bali lugha kali tu.

Kupitia hayo Team Tizneez ilipata wasaa mwema na Joh Makin tukazungumza juu ya mashabiki wa namna hii. Ambapo Joh Makin hakusita kutoa ushauri wake

Msikilize hapa chini.

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa