JINSI TEKNOLOJIA ILIVYOPIGA TAFU MZIKI WETU


Teknolojia ni kitu ambacho kimeendelea kukua kwa kasi hasa katika miaka ya hivi karibuni. Katika mziki tumeona jinsi ambavyo teknolojia imepiga tafu tasnia hii.

Katika miaka ya 90 ambapo Bongo Flava ilizaliwa, changamoto zilikuwa nyingi katika kuandaa mziki mpaka unapomfikia msikilizaji. Kesi za kazi kupotea kwa sababu ya computer kushambuliwa na Virus au Hard Disk kupoteza data zilikuwa nyingi. Hii haikuwa katika mziki tu lakini ni katika sekta zote ambazo zinatumia mfumo wa computer.

Lakini mambo sasa yamekuwa tofauti! Kampuni ya Microsoft imekuja na ufumbuzi wa shida zote zinazohusiana na upotevu wa data kwenye computer. Hii sio tu kwa watu wa mziki lakini pia kwa watu wote ambao wanategemea mfumo wa computer kufanya kazi.

Availability-on-Demand_thumb

Microsoft Azure inakuwezesha kuhifadhi na kufanya kazi yoyote ukiwa online. Huduma hii ni kwa watu binafsi hata makampuni. Unaweza kuhifadi nyaraka mbali mbali kama video, picha, sauti na hata maandishi. Microsoft Azure inakuhakikishia usalama na uhakika wa upatikanaji wa data zako muda wote  kupitia Computer, Tablet au Smartphone kwa kutumia username yako na password.

Dev-Digest-FI

Kwa wasanii na maproducer Microsoft Azure inawawezesha kuhifadhi nyimbo, midundo, picha za matukio pamoja na nyaraka. Pata uhakika na usalama wa nyaraka zako kuishi kwa muda mrefu zaidi bila kupotea.

Microsoft imeendelea kuhamasisha uzalishaji baada ya kuja na huduma ya Office 365. Kupitia Microsoft Office 365 unaweza kutembea na ofisi yako mkononi mwako. Achana na utamaduni wa kutembea na rundo la makaratasi, cd au external hard disk. Jiunge na huduma za kijanja za Microsoft Azure na Office 365 uishi kijanja. #DoMore