Je!Stamina ataenda tofauti na kauli za mdau na baadhi ya watangazaji?

Je!Stamina ataenda tofauti na kauli za mdau na baadhi ya watangazaji?

Leo ni siku ambayo msanii wa hiphop kutoka Moro Town Stamina anaachia wimbo wake akiwa na Maua Sama.

Stamina alijipatia umaarufu kupitia nyimbo kama Kabwela, Alisema, Panga pangua, Wazo la leo na nyingine nyingi.

Wimbi la wasanii wa hiphop kubadilika limekuwa kubwa kutokana na uongo wa wadau ambao umevikwa ukweli na baadhi ya watangazaji na wachambuzi wa muziki wa kizazi kipya kuwa hiphop haiuzi wala hailipi.

Ingawa wameshindwa kujua jambo dogo tu kuwa duniani kote hakuna muziki usiokuwa biashara. Maana ni wazi biashara yoyote inahitajia matangazo.

Hoja zao za hiphop haiuzi imefanikiwa kwa kiwango kikubwa maana wasanii wengi wa hiphop wamebadilika na kufanya makapuka mengi kila leo.

Je!stamina ataweza kuhimili kauli za mdau na watangazaji na kuendeleza aina yake ya muziki iliyompa heshima kwa watanzania?

Endelea kukaa nasi www.tizneez.com uwe wa kwanza kusikiliza wimbo huo ambao unaitwa Love me.

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment