Je!Kweli Belle 9 hapangiwa aina ya muziki na uongozi wake?

Je!Kweli Belle 9 hapangiwa aina ya muziki na uongozi wake?

Sauti sikiliza hapa Belle 9 akiongea na Team tizneez

Je!Kweli Belle 9 hapangiwa aina ya muziki na uongozi wake?

Maole ndiyo wimbo wake ambao unafanya vyema katika media kwasasa, wimbo huo ambao amefanya na msanii tokea kampuni ya Weusi ambaye ni Gnako.

Mabadiliko ya kimuziki juu ya msanii Belle 9 ni makubwa ukilinganisha na njia aliyotokea. Belle 9 ametambulika Zaidi katika uwanja wa Rnb tangu kutoka kwa wimbo wa Sumu ya penzi ambao ndiyo wimbo uliomtambulisha vyema kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Shauri zao ni wimbo wake wa mwisho kusimama katika muziki wa rnb, baada ya hapo kumefuata nyimbo mbili ambazo ni Give it to me na Maole ambazo ni aina tofauti na aina ya muziki ambao tumemzoea Belle 9.

Wengi wamekua wakiamini kuwa yote haya yanatokea shauri ya mabosi zake ambao wanasimamia muziki, licha ya Belle 9 kukanusha jambo hilo.

Belle amesema “Menejimenti inasimamia Zaidi biashara ila kwenye kurekodi ni mimi mwenyewe naselect kipi nifanye na beat gani nimeipenda,sababu muziki ni hisia ni sawa leo uniambie niimbe taarabu wakati sina hiyo mood itakuwa ngumu”.

Hivyo ni wazi kwa kauli zake Belle 9 hapangikiwi na uongozi wake, lakini je!nyimbo hizi alizotoa zimeweza kumuweka juu kimuziki?

Hili ni swali ni jambo la msingi la kutazama, neno mabadiliko ya muziki limetawala midomoni mwa wasanii na watangazaji wengi, ila jambo pekee la kujua ni kwamba “Sio kila mabadiliko lazima tuyafuate bali yale yenye maana na mafanikio”

Tuache maoni hapa

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez