Jcb Afunguka kuhusu Jay Mo

IMG_6954

Jcb Afunguka kuhusu Jay Mo

Jacob Makala ni moja kati wasanii wakongwe wa muziki wa hiphop wanaowakilisha vyema ramani ya Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Kupitia kipindi cha Ladha 3600 Jcb aliweka wazi mtazamo juu ya watu ambao wameendelea kumshambulia Jay mo katika hoja ya kukacha hiphop. Jcb amesema”Jay mo ameanza kutoa ngoma kali tangu miaka 2000, na amefanya mambo mengi kwenye muziki huu wa hiphop. Ila sijui wabongo wanataka nini au tuwape nini mpaka wamkubali Jay Mo.

Wimbo kama pesa ya madafu ni wimbo safi, sikiliza kuanzia ujumbe na hata flow. Na hakika ni wimbo ambao ni mzuri, ila kuna watu kadhaa wa media ndio huwa wanaongea tu na sio watu hata wa kununua cd au chochote kile. Hivyo kwangu ni wimbo safi na sioni kasaro yoyote

Maana hata kama ukichana kwenye beat tofauti na hiphop lazima uwezo wako uwe juu, yani ujue jinsi ya kupita katika beat hiyo.Sasa Jay Mo ameonyesha uwezo wake katika hilo

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez