JABIR SALEH SINA MASHAKA NA COUNTRY BOY

jabir

JABIR SALEH SINA MASHAKA NA COUNTRY BOY

Jabir Saleh ni moja kati ya watangazaji wachache ambao wana uwezo mkubwa katika kufahamu na hata uchambuzi juu ya muziki wa hiphop ndani na nje ya nchi.

Jabir ambaye sasa yupo katika kituo cha radio Efm, ambapo ni wiki mbili tu tangu aanze kutangaza kipindi kipya cha Ladha 3600. Kipindi ambacho kimeonekana kushika kwa kasi kubwa katika Jiji la Dar es salaam.

Jabir Saleh hakusita kuweka hisia zake kwa Country Boy ambapo alisema “Country Boy ni moja kati ya marapper vijana ambao nimekuwa nikiwafuatilia napenda kile anachokifanya, wapo vijana wengi walikuja lakini spidi imepungua. Umri wake bado unatoa nafasi kupasua kimataifa zaidi, na hata nikiambiwa kuweka hela kwa wasanii mimi nitaweka kwa Country mana sina mashaka Country Boy hasa katika uwezo wake kwwnye muziki.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez