Izzo Bizness Umesahau mzoea punda hapandi farasi?

Izzo Bizness Umesahau mzoea punda hapandi farasi?

‘Mzoea punda hapandi farasi’ msemo huu unaenda sawa na muziki wa kizazi kipya katika mlengo wa jinsi wasanii vile ambavyo wanaendesha muziki wao.

Katika uhalisia watangazaji na madj wamekuwa wazuri katika kazi ya kupokea Rushwa juu ya kucheza nyimbo za wasanii katika Radio na Runinga. Hali hii imepelekea wasanii wengi wengi kutumia njia hiyo ya kutoa rushwa ili tu aweze kuwa katika mzunguko wa nyimbo yake katika kituo cha radio na runinga husika.

Swala hili la rushwa limekuwa likizungumzwa na wasanii wengi katika vijiwe vyao na hata katika baadhi ya nyimbo zao. Na nguvu wanayotumia baadhi ya wasanii katika kutoa rushwa ilimradi wimbo wake uchezwe hata kama hauna vigezo ni kubwa mno.

Izzo Bizness ameingia katika kundi la wasanii ambao wamezungumzia rushwa, hii ni katika wimbo wake wa Dangorous Boy akiwa amemshirikisha Abela Music ambao kwa pamoja wanatengeneza The Amaizing.

Katika Verse ya pili hakusita kuandika “ Salute kwa madj wote mimi sihongwi nipigwe”

Swala la wasanii kuhonga kupigwa nyimbo zao katika vituo vya radio na runinga limekuwa ni jambo la kawaida, na sasa imegeuka kuwa ni maisha halisi ili uweze kupewa mzunguko wa nyimbo zako, ila tu  kama mkono wako utakuwa mfupi  basi sahau kupata mzunguko wa nyimbo zako.

Wasanii wengi unawasikia katika vituo vya radio na runinga hutumia pesa zaidi, jambo hili linapekea kila siku kuwasikia wale wale ambao unawasikia leo hii. Hii imetokana na mfumo mbovu ambao wasanii ndio chanzo cha hili, ambapo leo inaonyesha jinsi ambayo wamezoea kutoa rushwa ili tu wachezewe nyimbo zao katika vituo hivyo.

Jambo hili hakika linarudisha muziki nyuma badala ya kwenda mbele, maana wapo wasanii ambao hawaamini katika kutoa rushwa. Katika kukomesha hili ni lazima ukweli usemwe sio tu kusema pembeni.

Muda umefika wa kuweka ukweli juu ya hili swala la Rushwa.

Amka pinga rushwa kwenye muziki wa kizazi kipya wewe msanii.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez