Izzo Bizness Atangaza tarehe ya kutoa wimbo mpya.

Izzo Bizness Atangaza tarehe ya kutoa wimbo mpya.

Rapper kutoka Jijini Mbeya Izzo Bizness ambaye sasa anafanya vyema na crew yake ya The Amaizing akiwa na mshirika wake Abela,ambao wimbo kama Dangerous Boy uliweza kuwaweka kwenye chati za vituo vingi vya Runinga.

Ikumbukwe wimbo wa Dangerous Boy hakutoka audio bali video tu.

Mapema leo Izzo Bizness hakusita kuweka wazi tarehe na mwezi wa ngoma yake mpya kutoka. Ambapo Izzo Bizness amesema “Jumamosi hii tarehe 11-3-2016 ntaachia wimbo wangu mpya unaitwa SINUNUI STRESS Tanzania nzima 🙏🏽.

Izzo aliongeza kwa kusema “Ni ngoma ambayo naipenda sana, alafu pia ukizingatia sijafanya a rap song muda na pia kwasababu inagusa nyakati hizii,kaa tayari”

Facebook Tizneez

Twitter Tizneez

Youtube Tizneez

Instagram Tizneez