IZZO BIZNESS AFANYA KAZI NA BEN PAUL

e911f3bbdf8f1be20ea6c666e17bdbd8

Mkali tokea pande za Mbeya City Izzo Bizness ambaye shem lake ndiyo wimbo wake unaofanya vizuri katika upande wa audio na video aliyowashirikisha wakali G Nako na Mwana Fa.

Izzo ambaye wimbo wake wa kwanza kumtambulisha kwenye game ulikuwa ni Tenzi za mapenzi. Izzo amepost picha kupitia mtandao wa picha Instagram ambazo zimeonyesha akifanya kazi mpya na mkali Ben Paul.

Na hii itakuwa na kazi ya pili baada ya ile ya miss bizness iliyofanyika miaka kadhaa iliyopita ambayo iliwakutanisha.Licha ya kupost na kuonyesha kufanya kazi na Ben Paul pia mkali Izzo Bizness hakusita kuonyesha watayrishaji wa kazi hiyo ambao ni Master Jay pamoja na Dupy Beatz.

 

www.tizneez.com
Instagram tizneez
Facebook tizneez
Twtter tizneez