Hiphop Kwanza Concert ni mfano bora wa kuigwa.

images

Hiphop kwanza concert ni mfano bora wa kuigwa.

Malalamiko juu ya kubaniwa muziki wa hiphop kwenye vyombo vya habari yamekuwa makubwa kwa nyakati hizi. Ila katika uhalisia wasanii wa hiphop ni wasanii wenye nguvu katika jamii pia muziki wao.

Njia pekee ya kuokoa muziki huu na kutoa vilio vya wasanii wengi wa hiphop ni katika kuandaa matamasha yao binafsi bila kushirikisha mdau. Mimi ni moja ya watu ninao amini katika nguvu ya hiphop bila radio wala runinga.Wengi wao wamesahu muziki huu ulienea zaidi miaka ya 1990 mpaka mwaka 1995 hapa nchini bila kutumia radio wala runinga.

Sasa kwanini leo hii hiphop ishindwe kwenda mbele wakati kuna mitandao ya kijamii ambayo kama itatumika vyema itaweza kuwapa faida kwa wasanii hiphop.

Hiphop kwanza concert ni tamasha lililoandaliwa maeneo ya Mererani na litafanyika tarehe 31/7/2016 katika ukumbi wa Kwa Mdava Mererani muda ni kuanzia saa 3.00 usiku. Pia tamasha hili litashambuliwa na wasanii wengi wa hiphop akiwemo Mgosi Mkoloni, Mapacha Maujanja, Nikki Mbishi, Chindo, Chaba, Moplus, na wengine wengi.

Katika muziki wa hiphop ni mara chache sana kuandaa matamasha kama haya, hivyo hii iwe ni muendelezo isiishie Mererani tu bali na kwingineko lifike. Ila pia mashabiki wa hiphop wanapaswa kuudhulia kwa wingi katika matamasha haya ili kudhihilisha nguvu ya muziki huu kwa sasa ambao mdau na watu wachache wanaamini ni muziki ulishuka thamani.

Capture

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez