“Hiphop haina hela” Sheddy Clever

“Hiphop haina hela” Sheddy Clever

Merry You ya Diamond na Neyo ni kazi ya mikono yake inayofanya vyema sasa katika ramani ya muziki wa kizazi kipya,ikiwa ni ndani ya nchi na nje pia.

Sheddy Clever ni moja kati ya watayarishaji wazuri ambao tumebahatika kuwa nao katika muziki wetu. Licha ya kuweza kufanya kufanya nyimbo nyingi na nzuri,Sheddy hakuwahi kuweza kufanya wimbo wa hiphop na kuweza kufanya vyema kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Team tizneez ilizungumza na Sheddy Clever juu ya swala la kutokuwa  na wimbo wa hiphop ambao ameshawahi kuutengeneza na kuweza kufanya vyema kwenye Media.

Sheddy Clever Amesema “Kwanza wasanii wenyewe naamini kuwa hawana imani na mimi, na mimi nina ngoma nyingi tu za hiphop lakini sijazitoa. Ila pia hiphop haina hela ila muziki wa mapenzi una hela zaidi”

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Twitter Tizneez

Facebook Tizneez