Hii ni tofauti ya Ali Kiba na Diamond Platnumz.

01-Kiba+VS+Diamond

Hii ni tofauti ya Ali Kiba na Diamond Platnumz.

Kushindanishwa kati ya Ali Kiba na Diamond Platumz kumekuwepo katika kila mtaa ya wapenda muziki wa kizazi kipya. Hoja ni nyingi juu ya mashindano haya, ila sidhani kama kweli wenyewe wanashindana maana kila mmoja anaonekana kufanya kazi zake katika nafasi yake.

Team Tizneez tumeshaandika Makala nyingi kati ya Ali Kiba na Diamond, na katika kila Makala kila msanii amepewa chambuzi zake stahiki, ila team Tizneez hatujawahi kuwalinganisha hata siku moja.

Iko wazi wote ni wasanii wazuri na wanafanya vyema katika mataifa mengine duniani.

Ila moja ya vitu ambavyo tumegundua na tukaona tuna kila sababu ya kuandika ni tofauti moja ya kimuziki kati ya Diamond na Ali Kiba.

Tofauti hii imejikita katika nafasi ya muziki, na pia katika uwanja wa majukwaa tu. Leo hii katika matumbuizo yote ya Ali Kiba hufanya live, hata iwe tumbuizo la namna gani.

Hii inaonyesha ni jinsi gani muziki wake umekuwa, duniani kote kuimba live huonyesha umahiri wa msanii. Pia ni wakati muafaka wa Diamond Platnumz kuamka kifikra na kuanza kufanya matumbuizo ya live bila kutumia cd kama anavyofanya sasa.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez