‘Heri kufa macho kuliko kufa moyo’ Noorah

‘Heri kufa macho kuliko kufa moyo’ Noorah

Ice Cream ni moja kati ya nyimbo bora za wakati wote katika muziki wa kizazi kipya. Noorah ni mmiliki halali wa wimbo huu, lakini huwezi kuacha kusema ndiye msanii ambaye alileta swag za kiswanglishi.

Ukimya wake ni wa muda mrefu sasa, licha ya miaka 2 nyuma ambapo iliripotiwa alipata maradhi ambayo ilibidi kukaa nje ya muziki kwa muda fulani. Ila sasa afya yake imeimarika na hata juzi kuonekana jukwaani Mjini Shinyanga.

Haikunipa tabu kuzungumza na Noorah kuhusu ukimya wake pia swala la Chamber Squad kwa ujumla. Ambapo katika maelezo yake hakusita kusema “Muziki umebadilika kuliko muziki wa zamani, muziki wa sasa unahitaji nguvu ya kutosha na mtu mmoja peke yako huwezi kutosha. Inabidi uwe na timu ambayo itacheza kila upande yani mwingine hapa mwingine pale.

Hivyo mimi pekee yangu au niseme pia na Chamber Squad kwa ujumla tunatafuta watu wa kufanya nao kazi. Yani wasimame katika menejimenti na sisi tusimame katika utekelezaji wa kazi”

Wasanii wengi wamekua wakiamini msaada wa meneja zaidi na huamini kama meneja ndiye bosi, ila katika uhalisia msanii ndiye bosi. Noorah amekuwa akiamini hawawezi kufanya vyema bila ya kuwa na meneja, ilihali miaka kadhaa nyuma alifanya vyema katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Moyo wa kukata tamaa ndiyo ndio uliotawala katika nafsi ya Noorah. Ila kwa ukubwa wa kipaji chake kama anaamua kukufua moyo hakika nafasi yake ni kubwa katika muziki huu mwepesi wa sasa.

Amka Noorah Team Tizneez tunaamini  katika kipaji chako.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez