HARMONIZE “SIWEZI KUMSHAURI ALI KIBA”

12256753_463417153844508_1285195377_n

HARMONIZE “SIWEZI KUMSHAURI ALI KIBA”

Bado ni wimbo unaofanya vizuri sasa aliyomshirikisha msanii Diamond Platnumz, wimbo huo umefanyika katika Label ya WCB ambayo inamilikiwa na mkali Diamond Platnumz.

Hormonize ambaye sasa ameonekana kufanya media tour katika kusukuma kazi yake mbele zaidi, hata hivyo msanii huyu chipukizi ameendelea kuteka hisia za wengi hasa katika mahojiano anayokuwa anafanya kwa namna anavyotulia na kujibu maswali vizuri.

Harmonzie hakusita kujibu swali ambalo aliulizwa kama akikutana na Ali Kiba atamshuri kitu gani, ambapo Hormonize alisema “ Si rahisi mimi kumshauri Ali Kiba,pia naamini siwezi kumshauri Ali Kiba maana amenizidi katika mambo mengi, naweza kusema watu wakaona dogo vipi kaja juzi tu na anajifanya kunishauri, lakini kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii, pia afanye muziki mzuri maana ndio kitu cha msingi.”

Pia msanii Harmonize hakusita kuweka wazi kile kinachoonekana kuimba kama Diamond Platnumz ambapo alisema “siwezi kuimba kama Diamond hata mara moja, watu wananifananisha na Diamond maana nyimbo zinapoanza husikika neon Wasafii, pia kwakuwa wote tunaimba nyimbo za kulalamika, ila nadhani kwenye wimbo wa bado watu wamejua tofauti yangu na Diamond, Pia watu wajue kama tuko tofauti na Diamond hatufanani kwenye kuimba maana Diamond ni Diamond na dunia nzima inajua hilo”.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

 

 

Source Hatua Tatu Times fm tz