Harmonize Muziki bila kiki inawezekana.

sap

Harmonize Muziki bila kiki inawezekana.

Ni moja kati ya vichwa matata kutoka Wcb ambapo mpaka sasa Label hiyo ina wasanii wanne. Ambao ni Rich Mavoko, Ray Vany, Qeen Dorin na Harmonize.

Label hiyo inamilikwa na msanii Daimond Platnumz ambaye ni moja kati ya wasanii bora Afrika kwa sasa.

Kiki zilichukua nafasi katika miezi kadhaa nyuma ambapo tuliona wasanii wengi kabla ya kutoa wimbo walikuwa wakizusha mambo mengi yasiyo na msingi. Tuliona hata kundi la Yamoto Band kumtumia Aslay kumposti Ruby kwenye mtandao wa picha akiweka maelezo yenye utata ikionyesha kama ni mpenzi wake, lakini jambo hilo lilikuwa ni kiki ya wimbo wao wa “Suu”.

Tumeona leo Harmonize ametoa wimbo wake wa “Matatizo” ambao sio uliotoka kwa wengi kutarajia kama utatoka.

Hakika ni wimbo ambao umetoka na wapenda muziki wa kizazi kipya wameupokea kwa mikono miwili. Na katika muda mchache umeweza kuwa na watazamaji wengi katika mtandao wa youtube.

Hii inaonyesha ni jinsi gani kitu kikiwa kizuri hakihitaji kutumia nguvu za kiki. Ni vyema kujifunza kufanya muziki mzuri usiohitaji mambo ya kiki.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez