GihCue aonyesha ubora wake mbele ya Jux,Gnako, na Quick Racka

Capture

GihCue aonyesha ubora wake mbele ya Jux,Gnako na Quick Racka
Huyu ni director anaefanya vyema sasa katika anga ya muziki wa kizazi kipya hasa katika upande wa video. Ni wazi kila video inayotoka katika mikono yake basi huwa taofauti ni ile iliyopita.
Tangu kuanza kwa mwaka huu 2016 ameweza kutoa video mbili tu ambayo ni Bong Land na Hapo. Bongo land ni wimbo wa Hash Feat Kay ambao ni wazi wimbo huu umechezwa zaidi Trace kuliko hapa nchini. Hii inanifanya nione ni rahisi zaidi wimbo kuchezwa media za nje ya kama zikiwa na vigezo kuliko hapa ndani ambapo ni wazi muziki upo kirafiki, kimkoa, hata rushwa kutawala.
Hapo ni wimbo mpya wa Jux,Gnako ,Quick Racka. Ambapo audio yake imefanyika ndani ya Switcher Record lakini video yake imefanywa na GihCue muongozaji tokea Morogoro Mjini.
Iko wazi waongozaji wengi wa video hapa Tanzania huweka bajeti kubwa katika ufanyaji wa video, lakini husahau bajeti ya akili yake katika kufanikisha video husika. Katika video ya hapo tumeona bajeti ya akili aliyoweka Gihcue, hakika amefanya video nzuri . Naona tumefika mahala pazuri pakutumia waongozaji wa hapa hapa nyumbani
Team tizneez inakupongeza kwa kazi nzuri uliyofanya. Tunaamini katika uwezo wako.
www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez