“Game sio tena lile la ushindani siku hizi chuki, fitna na ukanda” Fid Q

Fid

“Game sio tena lile la ushindani siku hizi chuki, fitna na ukanda” Fid Q

Umkoa ni jambo ambalo msanii Nash mc amekuwa akilizungumza zaidi katika nyimbo zake hata mahoajiano machache ambayo huyafanya kwenye baadhi ya radio chache.

Mapema leo msanii Fid Q hakusita kuandika katika mtandao wa Twitter kupitia ukurasa wake, ambapo ameandika “Vijana wamebadilika sana sikuhizi,na hata GAME sio tena lile la enzi za ushindani wa skills tu, siku hizi fitna,chuki, na ukanda.

Hakika hili ni jambo ambalo Team tizneez tumekuwa tukiandika kila leo katika makala tofauti tofauti. Ni wazi muziki umekuwa ni wa kupendelewa kwa baadhi ya wasanii, watangazaji wapo kirafiki zaidi na sio tena kutazama nani ana wimbo mkali.

Hili ni jambo linalorudisha muziki nyuma zaidi, ni vyema kuacha tabia ya ukanda ambayo inaendelea kukua siku baada ya siku.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez