G SOLO AWATOLEA UVIVU WASANII WA BONGO FLEVA NA HIP HOP

300x300
Mmiliki wa studio za Kama kawa records G solo ambaye pia ni msanii wa muziki wa hip hop na mwandishi wa vitabu.Licha kuwa kimya katika muziki wake kwasasa lakini ameendelea kutoa mitazamo yake juu ya hali ya muziki pamoja siasa katika mtandao wa kijamii facebook.

Kupitia mtandao wa Facebook G Solo aliandika “Wasanii wa bongo fleva,mnaoimba na mnaojifanya kurap kwenye majukwaa ya harakati za mafisadi nyinyi ndo chanzo cha kuweka watanzania kwenye matatizo yanayoendelea kwenye nchi hii.

Wengi wenu mnaimba na kusifia ngono,starehe,mapenzi,hamuwezi kuwabadilisha watu kifikra na mitazamo na jinsi ya kujikwamua na hali ngumu ya maisha watanzania waliyonayo.

Inashangaza na kuchekesha kuona mnawasaliti hata waliowapigia kura hadi kufika hapo mlipo leo hii.Kitendo cha kusimama na kuwanadi viongozi ambao hata nyinyi mnajua sio,inadhihirisha wazi nyinyi mna njaa na upeo wenu wa akili ni mdogo hata kwenye kufikiri.

Mnashiriki kwenye kampeni wananchi wanaolia kwa ukosefu elimu bora,wananchi wanaolia kwa ukosefu wa afya bora rushwa imetawala,ufisadi uliokithiri,rasilimali za taifa zinauzwa kila kukicha na hata nyinyi ni wanafiki wakubwa kisa tu mnapata pesa ambazo hata hamtozikwa nazo

Hivi inamaana nyinyi kenge wote hamuoni watanzania wananavyolia? mbali na hao wanao imbaimba hata nyinyi mnaojiita hip hop nyinyi wote ni feki.Kupelekwa pelekwa kama ng’ombe ndio maana wengi wenu mnabebeshwa madawa ya kulevya nyinyi ni wasaliti na mnafaa hata kupigwa mawe huko kwenye kampeni.
Mwisho wenu unakuja.

Unaweza kuwa rafiki yetu facebook.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez