“Fid Q kumbuka kauli ya Nikki Mbishi juu ya ushauri wako”

“Fid Q kumbuka kauli ya Nikki Mbishi juu ya ushauri wako”

Fid Q ni moja kati ya wasanii wa hiphop wenye upana wa mawazo lakini heshima kubwa ndani ya muziki wa  hiphop na nje ya muziki huo.

Mara zote Fid Q huandika mambo mengi yenye changamoto maendeleo juu ya muziki hata nje ya muziki kwa maana ya katika maisha ya kila leo katika upande wowote ule na watu wote.

Mapema leo tumeona akiandika hisia zake juu ya watu ambao wamekuwa wakilaumu uwepo wa nguli wa mchezo wa mpira wa miguu David Beckham katika ardhi ya Tanzania na akiwa kimya bila ya kusema kama yupo katika ardhi hii tena katika kivutio cha hifadhi ya wanyama Serengeti.

Ambapo kupitia mtandao wa Twitter katika ukurasa wake Fid Q ameandika “Nimekuta watu wananung’unika juu ya suala zima la ujio wa DEVI mbugani kwetu eti kwasababu kila akipost hasemi kama yupo TZ mlimfadhili?”

Lakini Fid Q hakuishia hapo ambapo aliendelea kwa kuandika katika ukurasa wake huo wa Twitter “So ushauri wangu kama tunakimuhemuhe cha kupromotiwa ongeeni na serikali itupe hiyo kazi sisi kwanza halafu kisha ianze kuwafadhili hao”

Hakika ushauri wa Fid Q katika watu wahusika kuzungumza na Serikali na iwape wasanii kazi hiyo ni ushauri mzuri na wakuzingatiwa.

Ila ukirudi nyuma katika watu ambao walipaswa kulisema hili kila mara ni Baraza la Sanaa Tanzania (Basata). Maana kati ya lengo kuu au majukumu ya  kuanzishwa kwa BASATA ni ‘Kuishauri Serikali juu ya mambo yahusuyo maendeleo na uzalishaji wa kazi za Sanaa’

Je!Basata wanashauri Serikali juu ya umuhimu wa wasanii kutumika katika kutangaza vivutio tulivyonavyo hapa Tanzania?

Lakini siwezi kuacha kumpongeza Fid Q kwa ushauri wake huu wa watu kuzungumza na wahusika ili wasanii wapewe  kazi hiyo ya kutangaza vivutio vyetu, ila Fid Q anapaswa pia akumbuke kauli ya Nikki Mbishi.

Kupitia wimbo wa Natoka Tanzania wa Nikki Mbishi ambao ulitoka mwaka 2014 katika mstari wa kwanza amesema “Nchi ambayo haitambui mchango wa sanaa” katika uhalisia ni kweli nchi haitambui kabisa mchango wa Sanaa.

Yapo mengi ambayo kama kweli watatumia wasanii na Sanaa zao ni wazi manufaa mengi yatapatikana ila pia hata kuongeza kipato Zaidi kwa wasanii wetu na Sanaa zao kiujumla.

Lakini je!serikali yetu inaamini au kuthamini Sanaa zao na wasanii wenyewe kwa ujumla? Uhalisia ni hapana hivyo hatuna haja ya kutaka mtu atangaze yuko hapa ilihali sisi wenyewe hatuwezi kujitangaza kupitia wasanii au wana michezo wetu.

“Ni ya kheri upofu wa macho kuliko upofu wa akili”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa