Fid Q Aeleza sababu zilizomfanya kumtembelea mara nyingi Castro wakati akiwa kifungoni (Segerea)

maxresdefault

Fid Q Aeleza sababu zilizomfanya kumtazama mara nyingi Castro wakati akiwa kifungoni (Segerea)

Castro ni moja kati ya watarishaji wachache walioibuka miaka kadhaa nyuma. Wimbo wa Fid Q.com ni wimbo ulimpa heshima zaidi Castro pamoja na Fid Q.

Miaka kadhaa nyuma alikumbwa tuhuma za mauaji ya msanii mwenzake Steve 2k ambaye baadae Castro alihukumiwa kwenda jela kutumikia kifungo hicho.

Katika mazungumzo ambayo Team tizneez ilifanya mwaka 2013 baada ya kutoka jela kwa msamaha wa rais Castro hakusita kueleza juu msanii wa hiphop Fid Q.

Castro alisema “Kiukweli niwe muwazi nimekaa jela kwa miaka mingi mno, ila Fid Q ndiye msanii ambaye mara nyingi alikuwa anakuja kuniona pale Segerea na hata nilivyohamishiwa Ukonga. Jamaa yuko na moyo wa pekee sana hakika alikuwa akinipa faraja katika kipindi kile”

Team tizneez hakusita kumtafuta Fid Q kuzungumza machache juu ya hili ambapo alisema” Kwanza Castro alikuwa ni mshikaji wa Steve 2k mungu amlaze pema Steve 2k. Pia Castro alikuwa anamwabia Steve 2k anataka sana nifanye nae ngoma moja tu.

Kwa mara ya kwanza Studio ya Baucha mimi ndio nimefunga vifaa nikiwa na Snah Lee ambaye wengi wamemuita Snoop Lee, baada ya kufunga ikabidi tutengeneze kitu ndio ikabidi tutafute producer mmoja wa kupashia.

Na hapo ndipo Steve 2k akampigia Castro na akafika tukafanya kazi na kesho yake kwenda Radio ikawa hit song. Na kilichonifanya niende sana gerezani kumtazama ni kuwa Castro alinitengenezea ngoma ya kihistoria, hivyo ukimuongelea Fid q ni mtu anaebeba bendera ya muziki wa hiphop. Hii ilitokana na inspiration ya Castro kwa kutengeneza mdundo huo wa Fid q.com. Hivyo Castro na mimi tumetengenza manu script ya bongo hiphop. Hivyo nilikuwa na kila sababu ya kwenda kumuona wakati wote.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez