Ferooz Na malalamiko ya mdau.

Ferooz Na malalamiko ya mdau.

Shuka rhymes ni moja kati ya nyimbo bora zilizotoka miaka ya nyuma wakati wa kuchangamka kwa muziki wa kizazi kipya. Daz Dundaz ndio walikuwa wamiliki wa wimbo huu, huku production ikisimamiwa na P Funk Majani

Wakati huo muziki ulitawaliwa na jumbe zenye kubeba maisha ndani ya muziki na nje ya muziki pia. Tofauti na sasa pombe na ngono ndio mambo makuu yenye kusifiwa zaidi.

Katika uhalisia maisha ya mdau yamekuwa mazuri na hana malalamiko yoyote juu ya kipato akipatacho. Sugu aliwahi kusema “Kama wote tunaibiwa mbona wao hawalalamiki”

Ni wazi janja ya mdau ni kubwa mno, katika wimbo wa Shuka rhymes Ferooz hakisita kusema ” Jasho la msanii anaejenga ni mdau, twaimba sana lakini hatupati mafao wengi wetu tunabaki watu wa kupigana mizinga issue gani hizi”

Tangu kuimba maneno hayo katika wimbo wa shuka Rymes ni miaka takribani 10 imepita mpaka sasa, lakini kilio kutoka kwa wasanii kwenda kwa mdau kimeendelea kuwa kikubwa. Malalamiko ni mengi kwa upande wa msanii,  licha ya mdau kutumia nguvu kubwa kujisafisha.

Kuna kila sababu ya wasanii kuungana pamoja katika kutete maslahi yao, akili ziamke ni wazi mdau anawatumia vilivyo.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez