FAIZA ALLY “BIRTHDAY YANGU NATAKA IWE YENYE FAIDA”

images
Faiza Ally ambaye amejipatia umaarufu mkubwa hasa katika vituko mbalimbali anavyokuwa anafanya.Moja ya kituko chake ilikuwa ni kuvaa pampers siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa.Licha ya hivyo nyingine ni ile ya kuvaa nguo iliyomuacha wazi eneo kubwa la mwili wake.
Faiza Ally ambae ni mama wa mtoto mmoja ambaye mzazi mwenzake ni Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi.Kupita mtandao wa Facebook na Instagram Faiza aliandika kupitia ukurasa wake ambapo alisema “TANGAZOOOO December 17 ndio birthday yangu ntakua na miaka 32!!!!! nataka nifanye iwe yenye faida zaidi kwa watoto wanao hitaji- nitaweka kiingilio cha shilingi elfu 30 ntaanza kuuza hivi karibuni – na pesa hizo zitaenda kwa watoto yatima na watoto wanao hitaji misaada yetu….. Lkn pia tuta enjoy …. Tutakata keki – tutakunywa na kucheza mziki – tutapiga picha na kufahamiana zaidi…..kwa hivyo tuta enjoy na tutasaidia – pia ntaweka tiketi za VIP kwa sh elfu 50…. Na zitakua 20 tu! Nataka wewe umwambie mwenzio na mwenzio amwambie mwenzie- bila kusahau vivazi flan amazing.Tag rafiki yako na rafiki yako atag mwingine tuenjoy na huku tukitengeneza tabasamu kwa watoto wetu
na pia kwa yoyote atakae kuwa anasheherekea birthday yake na mm atakuja na keki yake tufurahi pamoja – hapo vipi?”Ameandika.
Facebook.com/Tizniz
Instagram.com/tizneez
Twitter.com/tizneez